Oct 02, 2022 13:48 UTC
  • Raisi: Njama za maadui za kuitenga Iran zimefeli

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama za karibuni za maadui za kutaka kutoa pigo kwa nchi hii na kueleza kuwa: Njama za maadui za kutaka Iran itengwe zimegonga mwamba.

Katika siku za karibuni wafanya fujo na waibua ghasia katika walikusanyika katika mitaa ya baadhi ya miji ya Iran na kuanza kuharibu mali za umma kwa kuchochewa  na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na zinazopinga Mapinduzi ya Kiislamu kwa kisingizio cha kifo cha Mahsa Amini.  

Wafanya fujo hao walikuwa wakichoma moto magari, pikipiki, mabenki na kuwashambulia askari usalama lengo likiwa ni kuzusha hofu na wasiwasi katika jamii.  

Ghasia nchini Iran baada ya kifo cha Mahsa Amini 

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja lengo la adui la kuratibu njama mpya dhidi ya Iran kuwa ni kutaka kuzuia maendeleo ya nchi hii na kuongeza kuwa: Adui ameingia katika medani kwa lengo la kuitenga Iran katika hali ambayo nchi hii iko katika mapambano ya kutatua matatizo ya kiuchumi na kujihuisha upya ili kuwa na mahudhurio makubwa zaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia na kimataifa; hata hivyo njama zote hizo zimefeli.  

Rais Raisi ameashiria makelele ya vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya Iran na vigezo vya undumakuwili vya nchi hizo na kueleza kuwa: Ijapokuwa suala la kuaga dunia Mahsa Amini linafuatiliwa kikamilifu na kwa umakini, na viongozi wote wamesisitiza suala hilo, lakini adui anajaribu kupotosha fikra za waliowengi kwa kuratibu hatua mbalimbali kupitia vyombo vya habari huku kundi la mabinti wa Kiafghani wakiuliwa na makundi ya kigaidi yanayopewa himaya na kuungwa mkono kwa hali na mali na Marekani, huku nchi hizo zinazodai kutetea haki za binadamu zikinyamaza kimya bila ya kuchukua hatua yoyote mbele ya mauaji hayo. 

Rais wa Jamhuri yya Kiislamu ya Iran amehoji kwamba, je katika mazingira kama haya kweli madai ya nchi za Magharibi ya kufuatialia haki za binadamu na haki za wanawake yanakubalika?