Oct 03, 2022 12:15 UTC
  • Kan'ani:  Iran na Marekani zabadilishana jumbe baina yazo pambizoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la UN

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa jumbe za uwakilishi za Iran na Marekani zilibadilishana jumbe kati yazo pambizoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Nasser Kan'ani leo Jumatatu amezungumza na vyombo vya habari katika mkutano wake wa kila wiki na kueleza kuwa: Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulikuwa fursa nzuri kwa ajili ya mazungumzo ya kuondoa vikwazo na kwamba Iran na Marekani zilibadilishana jumbe zao kupitia wapatanishi pambizoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.  

Ka'nani ameongeza kuwa, Mratibu wa upande wa Ulaya anaendelea na jitihada katika mazungumzo ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Iran inafungamana na majukumu yake ili kufikiwa mapatano mazuri na imara; ambapo Iran tayari imetoa jibu kwa rasimu ya majumuisho ya mwisho.  

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametuma salamu kwa mnasaba wa kukumbuka Siku ya Mshikamano na Watoto wa Palestina na kueleza kuwa utawala wa Kizayuni hadi sasa umewauwa shahidi watoto wa Kipalestina 2,230; jambo linaloonyesha umuhimu wa kupewa jina siku hii. 

Ukandamizaji na mauaji ya Israel dhidi ya watoto wa Palestina 

Tags