Oct 07, 2022 02:35 UTC
  • Brigedia Jenerali Ashtari: Usalama wa wananchi ni mstari wetu mwekundu

Kamanda wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa mtu au kundi lolote linalotaka kuvuruga na kuvuruga usalama wa watu, litakabiliwa na walinzi wa amani na usalama wa wananchi, na walinzi hao wa amani watakuwa pamoja bega kwa bega na wananchi.

Katika siku za karibuni waibua fujo na ghasia hapa nchini huku wakichochewa na vyombo vya habari vya maajinabi na vinavyopinga Mapinduzi ya Kiislamu, walijitokeza mitaani katika baadhi ya miji ya Iran na kuanza kuharibu mali za umma kwa kisingizio cha kuaga dunia msichana Mahsa Amini. 

Wafanya ghasia na uharibifu wa mali za umma 

Brigedia Jenerali Hossein Ashtari ameeleza kuwa fitina ya karibuni ilisambararishwa kwa kuwa macho wananchi na kutokana na miongozo ya Amiri Jeshi Mkuu na uwepo makini na nguvu ya vikosi vya usalama vya Iran.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni unaouwa watoto vimetangaza kuwa, utawala huo umeshindwa kutimiza malengo yake wakati huu na kwamba Iran ya Kiislamu imeweza  kudhibiti mikusanyiko hiyo na kuwatenganisha wananchi wa kawaida na wafanya ghasia na kuzima njama hizo. 

Kamanda wa Polisi ya Iran amesema kuwa, wananchi wamefanya vizuri sana katika fitna hiyo ya karibuni hapa nchini na waliweza kutofautisha njia ya haki na batili. Brigedia Jenerali Ashtari amesema: "Hii leo tuna amani na utulivu  nchini, na maadui waliokusudia kuvuruga usalama wamegonga mwamba."