Oct 07, 2022 11:48 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Ubeberu, Marekani, Uzayuni na Ukufurishaji zinapigana vita na haki na uadilifu visivyosuluhishika

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa: Uimwengu wa Ubeberu, Ulimwengu wa Uistikbari, Marekani, Uzayuni na kambi Ukufurushaji, zinapigana vita dhidi ya na haki na uadilifu visivyosuluhishika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Ayatullah Kazem Sediqi, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesema: tatizo la msingi ni kwamba, ulimwengu wa ubeberu, ulimwengu wa uistikbari, Marekani, Uzayuni pamoja na kambi ya ukufurishaji zinapigana vita visivyosuluhishika na haki, uadilifu na dini ya Mwenyezi Mungu; na tangu siku bendera ya dini ilipopandishwa na kupeperushwa katika ardhi ya Iran ulimwengu wa ubeberu umelifanya suala la kutekeleza njama, jinai na uhaini kuwa ndio ajenda yake kuu; na katika miaka hii 43, hakuna siku au fursa ambayo adui ameacha kuitumia kufanya uadui wake.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameongezea kwa kusema: "wananchi wameweza kuzima njama hizo moja baada ya nyingine, kuwashinda wafanyaji wake, na kuyahifadhi Mapinduzi."

Ayatullah Sedisi amekumbusha kuwa: kama alivyoeleza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika matukio haya kuna baadhi ya masuala madogo madogo na visingizio na kuna masuala makuu na ya msingi ambayo inapasa yazingatiwe kwa makini.
Kwa kutumia kisingizio cha kifo cha msichana Mahsa Amini, katika siku za karibuni, wafanya fujo na machafuko waliochochewa na vyombo vya habari vinavyopinga Mapinduzi na vyenye kinyongo na Jamhuri ya Kiislamu, walijitokeza mabarabarani na kufanya uharibifu mkubwa wa mali za umma katika baadhi ya miji ya Iran.../