Apr 15, 2017 02:29 UTC
  • Nchi za Kiarabu eneo la Ghuba ya Uajemi zinakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zinakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na kushuka mno kiwango cha ukuaji uchumi na matatizo mengi ya kifedha yanayozikabili nchi hizo.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, nchi za eneo la kusini mwa Ghuba ya Uajemi ambazo kwa muda sasa zimekuwa zikabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha na kupungua kwa vyanzo vyake vya fedha kutokana na kushuka bei ya mafuta katika masoko ya dunia, hivi sasa zinakabiliwa na tatizo la kushuka kiwango cha ukuaji wa uchumi.

Uzalishaji mafuta  hii leo hauna faida kwa mataifa ya Kiarabu

Habari zaidi zinaeleza kuwa, kutokana na hali hiyo, hivi sasa mataifa hayo yanakabiliwa na tatizo jengine la nakisi bajeti. Kwa mfano tu, kiwango cha ongezeko la uchumi wa taifa la Kuwait mwaka 2015 kilipungua kutoka asilimia 8 na kufikia asilimia tatu. Uchunguzi uliofanywa kuhusu hali ya mambo inayotawala katika uchumi wa mataifa ya kusini mwa Ghuba ya Uajemi unaonyesha kwamba, serikali za nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, zitaendelea kutekeleza siasa za mbinyo wa kifedha kwa raia wao kwa ajili ya kupunguza gharama za serikali hizo na kukabiliana na mwenendo wa mporomoko wa kiuchumi. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Saudia ni moja ya nchi ambazo zinakabiliwa na hali mbaya sana ya kiuchumi ambapo mdororo wa ndani wa uchumi wake umefikia asilimia tatu huku hali ikiendelea kuwa mbaya kila siku.

Rial ya Saudia namna inavyopoteza thamni yake

Hii ni katika hali ambayo, kabla ya hapo Saudia na nchi nyingine za eneo hilo zilipandisha gharama za umeme, mafuta na bei za gharama ya maisha. Kushupalia vita kunatajwa na weledi wa mambo kuwa sababu nyingine ya kuibuka matatizo ya kiuchumi katika nchi hizo za Kiarabu.

Tags

Maoni