Mar 24, 2018 15:31 UTC
  • Abdul-Malik al-Houthi: Israel imerejesha Yemen kundi la kishetani la Baha'i ili kuzusha fitina

Sayyid Abdul-Malik Badreddin al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Answarullah nchini Yemen, amesema kuwa kundi potofu la Baha'i limeanzisha tena harakati zake nchini humo ikiwas ni katika kuendelezwa vita laini vya adui wa dini ya Kiislamu.

Akifafanua kuwa kundi hilo lililopotea la Baha'i linapata uungaji mkono kamili kutoka kwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kwamba kwa sasa limeanzisha tena shughuli zake nchini Yemen, Houthi amefafanua kuwa, hivi sasa adui anatumia vita laini kujaribu kuwapigisha magoti raia wa Yemen.

Makao makuu ya kundi la Baha'i, huko Haifa ndani ya utawala haramu wa Israel

Aidha Katibu Mkuu huyo wa Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa utawala haramu wa Israel unaliunga mkono kundi hilo potofu kwa lengo la kupenya zaidi ndani ya ulimwengu wa Kiislamu na hatimaye kuzusha fitina baina ya Waislamu. Amesema, fikra za kishetani za Kibaha'i zinakusudia kutoa pigo kwa umma wa Kiislamu. Katika upande mwingine, kiongozi huyo wa Answarullah amewataka Wayemen kushiriki kwa kiwango kikubwa katika maandamano ya mwaka wa tatu wa kulaani uvamizi wa Marekani, Saudia na washirika wake dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu. Amesema, kushiriki kwa wingi katika maandamano hayo kutamuonesha adui uimara wa muqawama wa taifa hilo.

Wafuasi wa kundi la Baha'i wakiwa katika ibada

Katibu Mkuu wa Answarullah vile vile amesema kuwa, licha ya kupita miaka mitatu ya mauaji ya halaiki na uharibifu mkubwa unaofanywa na adui, lakini uvamizi huo umeshindwa kufikia malengo yake mbele ya muqawama wa Wayemen. Aidha amesema, taifa la Yemen litaendeleza muqawama kwa ajili ya kulinda heshima na utukufu wa nchi hiyo, na kuongeza kuwa, kushiriki kwa wingi wananchi katika maandamano hayo ya siku ya muqawama kwa mara nyingine kutaonesha umoja wa kitaifa dhidi ya adui Msaudi na madola ya Magharibi. Kundi potofu la Baha'i ni genge ambalo limekuwa likijinasibisha na Uislamu katika hali ambayo mafundisho yake yote yanakinzana sana na dini hiyo tukufu. Makao makuu ya genge hilo yako chini ya utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina la Israel.