Aug 28, 2018 03:32 UTC
  • Spika wa Bunge la Syria: Iran itakuwa pamoja na Syria katika kuikarabati nchi hiyo

Spika wa Bunge la Syria amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama ambavyo tangu mwanzoni mwa mgogoro wa nchi hiyo ilikuwa pamoja na wananchi na serikali ya Damascus, itashiriki pia katika ukarabati wa taifa hilo.

Spika Hammouda Sabbagh amesema hayo katika mazungumzo yake mjini Damascus na Mostafa Kavakebian, mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Bunge la Iran na kueleza kwamba, kipaumbele cha kwanza cha vikosi vya ulinzi vya Syria pamoja na washirika wake ni kung'oa kikamilifu mizizi ya ugaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Spika wa Bunge la Syria ameongeza kuwa, mwenendo wa kurejesha na kuimarisha amani na utulivu sambamba na kurejea wakimbizi wote wa nchi hiyo wa ndani na nje katika miji na vijiji vyao unaendelea vizuri.

Maeneo mengi ya Syria yameharibiwa vibaya na vita

Kwa upande wake, Mostafa Kavakebian mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Bunge la Iran ameashiria katika mazunguumzo yake na Spika wa Buunge la Syria uzushaji fitina wa Marekani na washirika wake katika eneo la Mashariki ya Kati na kueleza kwamba, kwa miaka mingi Syria imesimama kidete dhidi ya kambi ya Uistikbari na imefanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uwanja huo.

Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwa pamoja na taifa la Syria na itashiriki kwa nguvu zake zote katika kuikarabati nchi hiyo. 

Tags