Sep 11, 2019 12:23 UTC
  • Netanyahu atimua mbio kuelekea mafichoni akikwepa makombora ya wanamuqawama

Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni, vimeripoti habari ya kutimua mbio Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo, kufuatia kuvurumishwa na wanamuqawama wa Ukanda wa Gaza makombora yaliyovilenga vitongoji vya walowezi wa utawala huo.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari vya utawala wa Kizayuni, Netanyahu aliyekuwa ameshiriki katika hafla ya chama chake cha Likud katika kitongoji cha Ashdod, alilazimika kukatiza hotuba yake na kutimua mbio baada ya kusikika milio ya ving'ora vya hatari ya shambulizi la kombora na kuelekea mafichoni. Katika kujibu uchokozi wa utawala haramu wa Kizayuni, Jumanne ya jana wanamuqawama wa Palestina walifanya shambulizi dhidi ya vitongoji vya walowezi kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Baadhi ya makombora ya Hamas yanayowanyima usingizi viongozi wa Israel

Kabla ya hapo ndege za kivita, mizinga, helikopta na ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni, zilifanya mashambulizi katika wiki za hivi karibuni kwenye maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza. Inafaa kuashiria kuwa, utawala wa Kizayuni ulianzisha duru mpya ya mashambulizi ya anga dhidi ya eneo la Gaza tangu mwaka 2017, ambapo hadi sasa maelfu ya raia wa eneo hilo wameuawa shahidi na kujeruhiwa. Aidha tangu mwaka 2007 utawala huo umekuwa ukitekeleza mzingiro wa kila upande sambamba na kuzuia kuingia bidhaa muhimu yakiwemo madawa, katika ukanda huo.

Tags

Maoni