Sep 12, 2019 04:16 UTC
  • Muhusika mkuu wa mauaji ya ndugu ya Katibu Mkuu wa Answarullah aangamizwa

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Wokovo wa Kitaifa nchini Yemen imesema kuwa, Mohammad Ali Ghayd Zawi, muhusika mkuu wa mauaji ya Ibrahim Badruddin Al Houthi, ndugu ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah nchini Yemen ameangamizwa.

Ibrahim Badruddin Al Houthi, ndugu ya Abdul-Malik Badreddin al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Answarullah, aliuawa shahidi tarehe 11 Agosti na vibaraka wa muungano vamizi wa Saudi Arabia. Aidha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa nchini Yemen imeongeza kwamba, uchunguzi uliofanywa na vyombo vya usalama, ulithibitisha kwamba Zawi mwenye umri wa miaka 54 alikuwa na uhusiano na idara ya usalama ya Saudia. Inafaa kuashiria kuwa, katika miezi ya hivi karibuni, Saudia na baada ya kushindwa kwake katika ulingo wa vita na kisiasa, ilianzisha mbinu chafu ya kuwaua kigaidi viongozi wa Yemen. Jinai hiyo inatekelezwa na vibaraka wa Riyadh waliopo nchini Yemen. 

Harakati ya Answarullah iliyolipiza kisasi

Wakati huo huo, kwa akali vibaraka 7 wa Saudia wameangamizwa na jeshi la Yemen kwa kushikiriana na harakati ya Answarullah katika jimbo la Hajjah, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Kanali ya Al-Masirahh ya Yemen imetangaza kwamba vobaraka hao wa Saudia waliangamizwa jana katika operesheni iliyofanywa na kikosi cha kulenga shabaha cha jeshi na kamati za wananchi na katika kambi mbili za al-Matun na al-Salbah za mkoa wa Hajjah. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni Mohamed al-Atifi, Waziri wa Ulinzi wa Yemen alitahadharisha kwamba jeshi la nchi hiyo litaigeuza nchi hiyo kuwa jahannam kwa nchi wavamizi.

Tags

Maoni