Sep 17, 2019 13:07 UTC
  • Rais Tayyip Erdoğan akosoa vikali mwendelezo wa mashambulizi ya Saudia nchini Yemen

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ametoa radiamali yake kufuatia mashambulizi ya Wayemen dhidi ya taasisi za mafuta za Saudia (ARAMCO) na kusema kuwa ni lazima kukumbuka ni nani aliyeanzisha hujuma za kijeshi dhidi ya Yemen.

Rais Erdoğan ameyasema hayo mbele ya waandishi habari mwishoni mwa kikao cha nchi zinazodhamini usitishaji vita nchini Syria yaani Russia, Iran na Uturuki na ambacho kimefanyika mjini Ankara kupitia mazungumzo ya Astana, mji mkuu wa Kazakhstan. Amesema kuwa mashambulizi ya muungano wa Saudia dhidi ya raia wa Yemen ni lazima yasitishwe na kuanza ukarabati ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Baada ya kujiri shambulizi dhidi ya Shirika la Mafuta la Saudia ARAMCO

Hii ni katika hali ambayo mwishoni mwa kikao hicho cha ngazi ya marais wa nchi zinazounga mkono mwenendo wa mazungumzo ya Astana (yaani Iran, Russia na Uturuki), kumesisitizwa suala la kulindwa umoja wa ardhi yote ya Syria. Saudia kwa uungaji mkono wa Marekani, Imarati na nchi nyingine ilianzisha mashambulizi yake nchini Yemen kuanzia mwezi Machi 2015, sambamba na kuizingira kila upande nchi hiyo. Hadi sasa vita hivyo vya kila siku vya Saudia na washirika wake nchini Yemen vimepelekea zaidi ya watu elfu 16 kuuawa, na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa, kama ambavyo pia mamilioni ya watu wamelazimika kuwa wakimbizi.

Maoni