Sep 19, 2019 07:03 UTC
  • Jeshi la Kuwait lajiweka tayari kukabiliana na tukio lolote katika eneo

Jeshi la Kuwait limetoa taarifa na kueleza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hivyo vimeajiandaa kukabiliana na matukio na tishio lolote katika eneo.

Kamandi ya vikosi vya jeshi la ulinzi la Kuwait imetangaza kuwa baadhi ya askari jeshi wanajiandaa katika kiwango cha juu na uwezo mkubwa wa makabiliano kwa kuzingatia hali ya msuguano inayotawala nchini humo  na katika eneo kwa ujumla. Imesema kuwa askari hao hivi sasa wanafanya mazoezi ya anga na baharini. 

Vifaru vya Kuwait vikiwa tayari kukabiliana na tishio lolote
 

Jeshi la Kuwait aidha limesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kulinda amani na umoja wa ardhi yote ya nchi hiyo na kuwatolea wito wananchi kupuuza uvumi uliosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari visivyo rasmi.  

Viongozi wa Kuwait wamekumbwa na wasiwasi baada ya jeshi la Yemen na wanamuqawama wa nchi hiyo kushambulia kwa droni vituo vya mafuta vya Aramco nchini Saudi Arabia na pia kuonekana droni moja ikiruka katika anga ya kasri ya Mfalme wa Kuwait. 

Tags