Oct 20, 2019 11:57 UTC
  • Maandamano Lebanon; Samir Jaja atangaza kujiuzulu serikalini mawaziri wa chama chake

Samir Jaja mkuu wa chama cha Lebanese Forces amesema kuwa, serikali ya sasa ya Lebanon haina uwezo wa kuchukua hatua za lazima ili kuboresha hali ya uchumi wa nchi hiyo, hivyo ametaka kujiuzulu mawaziri wa chama chake serikalini.

Samir Jaja amekadhibisha kufikiwa matapatano yoyote na Saad Hariri Waziri Mkuu wa Lebanon kuhusu kujiuzulu mawaziri wa chama chake na akasema amewataka mawaziri wake kutoka chama cha Lebanese Forces wajiuzulu serikalini. Chama cha Lebanese Forces kina mawaziri wanne katika serikali ya mseto ya Lebanon. 

Jaja amebainisha kuwa, hana imani na serikali ya sasa ya Lebanon na kuongeza kuwa, viongozi husika hawana dhamira na irada ya kweli ya kuyapatia ufumbuzi matatizo ya sasa ya nchi hiyo. Miji mbalimbali ya Lebanon khususan mji mkuu Beirut tangu Alhamisi iliyopita imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali mbaya ya uchumi na vile vile kupanda kwa kodi katika huduma zinazotolewa na serikali ikiwemo ya intaneti.

Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon jana katika Marasimu Makubwa ya Waliosalia Nyuma katika Arubaini ya Hussein (a.s) ameitaka serikali kutowachochea wananchi maskini kwa kuwatwisha kodi mpya. 

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon 
 

 

Maoni