Oct 21, 2019 12:27 UTC
  • Makundi ya muqawama Palestina yaonya kuhusu hatua za Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa

Makundi ya wanamuqawama wa Palestina yametoa onyo kwa hatua za utawala haramu wa Israel dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu.

Taarifa ya makundi hayo ya mapambano ya Palestina imeeleza kuwa, hatua za utawala haramu wa Israel za kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqswa hazitabakia bila majibu.

Kadhalika makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina yamezituhumu baadhi ya nchi za Kiarabu yakisema kwamba, zimekuwa zikihusika katika mashambulio na hujuma mtawalia za walowezi wa Kizayuni za kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, kuendelea mashambulio na hujuma za Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa kutapelekea kuwaka moto ambao utawala dhalimu wa Israel ndiyo utakaoungua kwa moto huo. 

Wanajeshi wa Israel wakivamia Msikiti wa al-Aqswa

Kadhalika makundi ya mapambano ya Palestina yamelaani safari ya ujumbe wa Israel huko Bahrain kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa usalama wa baharinina na kuzitaka nchi za Kiarabu kukataa mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqswa na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.

Uvamizi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina. 

Tags

Maoni