Oct 22, 2019 11:46 UTC
  • Jeshi la Iraq: Askari wa Marekani hawana haki ya kuwepo ndani ya nchi hii

Kamandi ya jeshi la Iraq sambamba na kutoa taarifa imesema kuwa, askari wa Marekani ambao wametokea Syria, wanaweza tu kuitumia Iraq kama njia ya kuvuka na kwamba hawana haki ya kuweka kambi nchini humo.

Taarifa hiyo ya kamandi ya jeshi la Iraq imesisitiza kuwa, askari hao wa Kimarekani ambao wametokea Syria, wanaweza tu kuingia katika jimbo la Kurdistan na kutumia njia hiyo kwa ajili ya kuvuka Iraq, na kwamba hawana kibali cha kubakia ndani ya nchi hiyo. Vyombo vya habari pia vimetangaza kwamba, zaidi ya magari 100 ya deraya ya askari wa Marekani yameondoka Syria na kuingia Iraq. Aidha afisa mmoja wa usalama wa jeshi la Iraq Jumatatu ya jana alitoa habari ya kuingia nchini humo askari 1000 wa Marekani kutokea Syria kupitia mkoa wa Nainawa kaskazini mwa Iraq.

Askari vamizi wa Marekani eneo la Asia Magharibi

Wakati huo huo Karim al-Muhammadawi, mjumbe wa kamisheni ya usalama na ulinzi katika bunge la Iraq amesema kuwa, Washington inafanya njama ya kuwarejesha tena wanachama wa kundi hatari la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), kwa kuwahamisha askari wake kutoka Syria na kuwaingiza Iraq.

Tags

Maoni