Oct 22, 2019 11:55 UTC
  • Rais Bashar al Assad atembelea mstari wa mbele wa vita dhidi ya magaidi kusini mwa Idlib

Rais Bashar al Assad wa Syria akiwa pamoja na makamanda wa jeshi la nchi hiyo, amefika katika mstari wa mbele wa vita dhidi ya makundi ya kigaidi katika mkoa wa Idlib.

Ofisi ya rais wa Syria imeripoti leo Jumanne kwamba, Rais Assad alikuwa ameenda mkoa wa Idlib kwa ajili ya kulitembelea jeshi katika eneo la Hobait, kusini mwa mkoa huo. Itakumbukwa kuwa mkoa wa Idlib ni mji pekee nchini Syria ambao bado unadhibitiwa na makundi ya kigaidi pamoja na wanamgambo wanaobeba silaha ambao wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki. Habari nyingine ni kwamba jeshi la Syria na katika hatua yake ya kuweka kambi maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, asubuhi ya leo limeingia katika vijiji saba vingine kaskazini magharibi mwa mkoa wa Al-Hasakah.

Rais Bashar al Assad wa Syria akiwa na makamanda wa jeshi huko Idlib

Katika upande wa pili, duru za habari nchini Syria zimetangaza kwamba jeshi la nchi hiyo linakusudia kupiga kambi kaskazini mwa mkoa wa al-Hasakah. Itakumbukwa kuwa baada ya jeshi la Uturuki kuanzisha mashambulizi kaskazini mwa Syria hapo tarehe 9 Oktoba na baada ya Marekani kuwafanyia hiyana wanamgambo wa Kikurdi, tarehe 13 ya mwezi huu wanamgambo hao walitiliana saini na serikali ya Damascus wakilitaka jeshi la nchi hiyo kuwalinda kutokana na hujuma za Uturuki.

Tags

Maoni