Nov 16, 2019 07:52 UTC
  • Wazayuni waendelea kushambulia Ghaza licha ya makubaliano ya kusitisha vita

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni mapema leo asubuhi zimefanya mashambulizi mengine katika Ukanda wa Ghaza licha ya Israel yenyewe kuomba usitishaji vita na wanamuqawama wa Palestina.

Ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia kwa makombora 9 kituo cha polisi wa baharini cha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika Ukanda wa Ghaza.

Avichay Adraee, msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amedai kuwa eti mashambulizi hayo yamefanyika baada ya kurushwa maroketi kutoka Ukanda wa Ghaza yaliyopiga kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Be'er al Sab'e.

Wahanga wakubwa wa jinai za Israel ni wanawake na watoto wadogo wa Kipalestina

 

Mashambulizi hayo yamefanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina licha ya kwamba tarehe 14 mwezi huu yaani siku ya Alkhamisi, utawala wa Kizayuni ulifikia makubaliano ya kusimamisha vita na harakati ya Jihadul Islami ya Palestina kwa upatanishi wa Misri.

Mashambulizi ya hivi sasa ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza yalianza asubuhi ya siku ya Jumanne ya taehe 12 Novemba, 2019.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa idadi ya wananchi wa Palesitna waliouawa shahidi kutokana na uvamizi huu mpya wa utawala katili wa Israel imefikia watu 34 na zaidi ya 100 wamejeruhiwa.

Tags

Maoni