Nov 16, 2019 12:29 UTC
  • Wakazi wa Haifa waandamana kuiunga mkono Gaza

Wapalestina wanaoishi Haifa ndani ya utawala haramu wa Israel, wamefanya maandamano kuunga mkono wakazi wa Ukanda wa Gaza kutokana na jinai za Tel Aviv.

Maandamano hayo ambayo ni katika mfululizo wa maandamano ya wakazi wa maeneo tofauti ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, yameshika kasi na kuingia Haifa. Washiriki wa maandamano hayo sambamba na kulaani vikali mashambulizi ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya eneo la Gaza, wamepiga nara kama vile za 'Enyi watu wa Gaza endelezeni muqawama na kuweni imara', 'Enyi wakazi wa Gaza kuweni wenye nguvu na irada yenye nguvu,' 'Enyi wakazi wa Gaza endeleeni kuwa imara, wenye izza na utukufu' na 'Gaza kuweni imara mithili ya upanga.'

Wakazi wa Gaza wakilia kwa uchungu kufuatia ndugu zao kuuawa kinyama na Israel

Inafaa kuashiria kuwa Jumanne asubuhi utawala haramu wa Israel ulianzisha duru mpya ya mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya eneo hilo. Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kwamba katika mashambulizi hayo mapya ya utawala wa Kizayuni katika eneo la Gaza jumla ya Wapalestina 34 wameuawa shahidi wakiwemo wanafunzi sita na mwanamke mmoja. Aidha zaidi ya wengine 110 wamejeruhiwa ambapo kati yao ni wanawake na watoto wadogo.

Tags

Maoni