Nov 20, 2019 07:06 UTC
  • Pentagon: Uwezo wa makombora wa Iran ndio mkubwa zaidi M/Kati

Utafiti uliofanywa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) unaonyesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo nchi yenye uwezo mkubwa zaidi katika uga wa makombora ya balistiki katika eneo la Asia Magharibi.

Pentagon imekiri kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii imepiga hatua kubwa sana katika masuala ya ulinzi hasa upande wa nguvu za makombora licha ya jitihada chungu nzima za kuzima au kupunguza uwezo huo.

Afisa mmoja wa Idara ya Kiitelijensia ya Marekani ambaye hakutaka kutaja jina lake amefichua kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulijumuishwa pia kwenye utaftiti huo wa Pentagon.

Kadhalika Pentagon imekariri madai yake ya kila siku kwenye ripoti hiyo kuwa mradi wa makombora wa Iran sio wa amani wala kujihami, na kwamba makombora ya Iran yenye uwezo wa kupiga hadi kilomita 2000 yanaweza kufika Tel Aviv na Riyadh.

Aina kadhaa za makombora ya Iran

Hivi karibuni, Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH alisema: "Leo hii tumefanikiwa kuzalisha makombora ya kupiga vyombo vya baharini kutokea fukweni na kwamba makombora yote ya Iran kuanzia yale ya kilomita 200 hadi yale ya kilomita 2000 yanapiga shabaha kwa ustadi mkubwa sana."

Uwezo huo wa Iran wa makombora umeifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa na jeshi imara ambalo hata maadui wanalazimika kukiri uwezo wake wa kujihami.

Tags

Maoni