Nov 21, 2019 12:25 UTC
  • Benny Gantz: Netanyahu ndiye anakwamisha mazungumzo

Baada ya kushindwa kuunda serikali ndani ya utawala haramu wa Kizayuni kwa mara nyingine Benny Gantz amemtuhumu Benjamin Netanyahu kwamba anakwamisha mazungumzo kuhusiana na kadhia hiyo.

Baada ya Gantz, kiongozi wa muungano wa Blue and White Alliance kushindwa kuunda serikali mpya, vyama vya kisiasa ndani ya utawala wa Kizayuni vitakuwa na muhuma wa siku 21 za kumuunga mkono Netanyahu, Benny Gantz au mgombe mwingine wa tatu kwa ajili ya kuunda serikali na kinyume na hivyo kutaitishwa uchaguzi mwingine kwa mara ya tatu katika kipindi cha mwaka mmoja. Kwa mujibu wa habari hiyo, baada ya Gantz kushindwa kuunda serikali amezungumzia muhula wa siku 21 kupitia kikao na waandishi wa habari mjini Tel Aviv na kusema kuwa, Benjamin Netanyahu amekuwa akikwamisha mambo katika mazungumzo ya kuunda serikali.

Netanyahu ambaye amekataa kutii takwa la raia wa Israel ambao hawamtaki kuendelea kuwa waziri mkuu

Ameongeza kwamba Waziri Mkuu  huyo wa Israel sambamba na kufanya juhudi za kijeuri za ukwamishaji mambo, anafumbia macho uamuzi wa wananchi ili aendelee kubakia madarakani. Kiongozi huyo wa muungano wa Blue and White Alliance ameendelea kufafanua kuwa watu wengi waliopiga kura walitaka kupunguzwa madaraka ya viongozi wa mrengo wa kufurutu ada sambamba na kujitenga mbali na njia iliyofuatwa kwa miaka mingi na Benjamin Netanyahu ingawa hata hivyo waziri mkuu huyo haamini uamuzi wa wananchi.

Maoni