Nov 21, 2019 12:30 UTC
  • Saudia yakaribisha uamuzi wa Marekani kuhusiana na Fordo

Serikali ya Saudi Arabia imekaribisha uamuzi wa Marekani wa kuhitimisha msamaha wa vikwazo kuhusiana na ushirikiano wa nyuklia na Iran katika kituo cha Fordo.

Jana chanzo kimoja katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia kililiambia shirika rasmi la nchi hiyo la WAS kuwa, serikali ya Riyadh imekaribisha uamuzi wa Marekani kuhusiana na taasisi ya nyuklia ya Fordo. Jumatatu iliyopita Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani sambamba na kukariri tuhuma zake zisizo na msingi wowote dhidi ya miradi ya amani ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa, Washington itafuta msamaha wa vikwazo unaohusu ushirikiano wa sekta ya nyuklia na Iran katika taasisi ya nyuklia ya Shahidi Masoud Alimohammadi ya Fordo. Aidha tarehe tatu Mei mwaka huu serikali ya Marekani pia ilifuta misamaha mitatu ya ushirikiano wa nyuklia na Iran kukiwemo kuhamisha urani iliyorutubishwa pamoja na maji mazito kwenda nje ya nchi.

Pande tatu zinazokula njama dhidi ya Iran

Hii ni katika hali ambayo hatua hizo zinakinzana kikamilifu na vipengee vya makubaliano ya JCPOA pamoja na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ushirikiano wa miradi ya amani ya nyuklia ya Iran, unafanyika kupitia moja ya vipengee vya makubaliano ya JCPOA. Tangu mwanzoni mwa kutekelezwa makubaliano ya JCPOA yaani tarehe 16 Januari 2016 serikali ya Marekani ilianza hatua za ukwamishaji mambo katika utekelezaji wa makubaliano hayo sambamba na kufanya njama za kupunguza maslahi ya kiuchumi ya Iran katika mapatano hayo. Aidha ukwamishaji mambo huo ulishtadi baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump.

Maoni