Dec 05, 2019 08:08 UTC
  • Hamas: Madai ya usitishaji vita wa muda mrefu ni propaganda za uchaguzi za utawala wa Kizayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaja tetesi iliyoenea katika vyombo vya habari vya Kizayuni kuhusu jitihada za utawala huo za kufikia makubaliano ya usitishaji vita ya muda mrefu na Ukanda wa Ghaza kuwa ni propaganda za uchaguzi.

Khalil al Hayya mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amepinga tetesi hiyo na kueleza kuwa Hamas haikubali mapendekezo kama hayo madhali maghasibu hao wa Kizayuni hawaheshimu na kutekeleza makubaliano yao kuhusu kusitisha mapigano na kuondoa mzingiro huko Ghaza. 

Al Hayya amesisitiza kuwa mazungumzo yanayoendelea sasa kati ya Hamas na Misri huko Cairo yanafanyika lengo likiwa ni kuchunguza masuala yanayoihusu Palestina likiwemo suala la kufanyika uchaguzi na mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina.   

Ujumbe wa ngazi ya juu wa harakati ya Hamas chini ya uongozi wa Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo Jumatatu wiki hii ulifanya safari mjini Cairo ili kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Palestina. Wakati huo huo  ujumbe wa harakati ya Jihadul Islami pia umewasili Cairo ukiongozwa na Ziad al Nakhalah Katibu Mkuu wa harakati hiyo. 

Ziad al Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihadul Islami

Tags

Maoni