Dec 10, 2019 08:10 UTC
  • Zarif: Iran iko tayari kusaidia mchakato wa kurejesha amani na usalama katika eneo

"Kuwepo kwa majeshi ya nchi za kigeni katika eneo la Asia Magharibi hakujaimarisha Amani na usalama katika eneo hili."

Matamshi hayo yalitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif katika Mkutano wa 8 wa "Moyo wa Asia" wa Mawaziri wa Mambo ya Nje mjini Istanbul, Uturuki ambako alibainisha mitazamo ya Iran kuhusiana na suala la amani katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Tajiriba na uzoefu unaonesha kuwa, Marekani kamwe haina nia ya kuimarisha amani na usalama au kung'oa mizizi ya ugaidi katika eneo. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa, Marekani yenyewe ndiyo sababu ya mizozo, migogoro na vita vya miongo kadhaa ya hivi karibuni katika eneo la m Asia Magharibi ikiwemo Afghanistan.

Akihutubia mkutano wa Istanbul, Muhammad Javad Zarif ameunga mkono mchakato wa kurejesha amani nchini Afghanistan chini ya usimamizi na uongozi wa Waafghani wenyewe na kwa kushirikishwa makundi na mirengo yote ya kisiasa likiwemo kundi la Taliban. Ameongeza kuwa kuna ulazima wa kutumia nyenzo zote zinazowekana kwa ajili ya kusahilisha mchakato wa kurejesha amani na kulinda matunda ya mkutano wa mwaka 2001 wa Born na khususan katika fremu ya Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan ukiwa msingi wenye nguvu kwa ajili ya kufikia njia yoyote ya ufumbuzi wa kisiasa.  

Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika Mkutano wa 8 wa Moyo wa Asia mjini Istanbul Uturuki

Matamshi hayo ya Zarif katika Mkutano wa Istanbul ni ishara ya moja kwa moja ya vitisho vilivyosababishwa katika eneo la Asia Magharibi kutokana na siasa za uingiliaji kati za nchi ajinabi. Kuhusiana na suala hilo Zarif amesema: Vitisho vikubwa vya Daesh huko Afghanistan ambavyo vimepelekea damu nyingi kumwagika na kuenea mielekeo hatari ya uchupaji mipaka havipasi kusahauliwa. Kuenea kwa vitisho hivyo huko Afghanistan na katika Asia ya Kati hakutakuwa kwa maslahi kwa nchi hizo  kama ambavyo hakuna yoyote aliyenufaika na kuanzishwa na kuungwa mkono Daesh na makundi mengine yenye misimamo mikali huko Syria na Iraq. Mchakato huu unapaswa kusitishwa kabla ya kujiri maafa makubwa.  

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha mara kadhaa katika hotuba zake kwamba Marekani haina uwezo wa kudhamini usalama katika eneo. Mfano wa wazi wa uhakika huu wa mambo ni kuweko nchini Afghanistan Marekani kwa muda wa miaka 14 ambako si tu hakujaleta amani kwa wananchi wa Afghanistan bali  kumeifanya hali ya usalama kuwa mbaya zaidi. 

Katika mazingira kama hayo kuharakishwa juhudi za kieneo na kimataifa kwa ajili ya kurejesha amani huko Afghanistan ni njia pekee itakayosaidia kuondokana na changamoto za kiusalama katika eneo. Katika uwanja huu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijaacha kuisaidia Afghanistan ili kupunguza matatizo ya wananchi.  

Wakati huo huo Iran imekuwa na nafasi na mchango wa hali ya juu katika kuwezesha ufikiwaji rahisi wa njia za mawasilianao na kutoa huduma na misaada ya kimaendeleo na kiuchumi; na pia kwa miongo kadhaa imekuwa mwenyeji wa wakimbizi wa Kiafghani kwa kuwadhaminia masomo na huduma za afya na matibabu. Kama ambavyo Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukipongeza na kushukuru juhudi zinazofanywa na Iran katika kuisaidia Afghanistan. 

Iran aidha imeandaa suhula mbalimbali ikiwemo ufikaji haraka katika maji ya kimataifa kupitia bandari ya kistratejia ya Chabahar katika kusaidia uchumi na maisha ya wananchi wa Afghanistan. Hivi sasa pia inakamilisha ujenzi wa njia ya reli ya Chabahar hadi Zaidan kama sehemu muhimu ya korido ya kaskazini-kusini. Njia hiyo ya reli inaziunganisha Afghanistan na nchi za Asia ya Kati kupitia Chabahar hadi katika maji huru. Si hayo tu, bali Iran iko tayari kushirikiana na pande zote zenye lengo la kufanikisha amani katika eneo. Kwa kuzingatia hayo yote, hotuba ya jana ya Zarif katika Mkutano wa Moyo barani Asia huko Istanbul ni sisitizo la mara nyingine tena kuhusu mitazamo ya wazi ya Iran kwa lengo ya kuunga mkono na kuwezesha upatikanaji wa njia za kurejesha amani na usalama katika Asia Magharibi.  

Bandari ya kistratejia ya Chabahar
Maoni