Dec 13, 2019 10:29 UTC
  • Syria yakosoa jinai zinazofanywa na Marekani dhidi ya binadamu na haki zake

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeikosoa Marekani kutokana na jinai zake dhidi ya ubinadamu na haki za binadamu katika maeneo mbalimbali ya dunia na imetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na jinai hizo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 70 wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu imezungumzia jinai na uhalifu unaofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani nchini humo na kusema: Hadi sasa muungano huo umeua maelfu ya raia wasio na hatia nchini Syria ikiwa ni pamoja na maeneo ya Deir al-Zour na Raqqah.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2014 Marekani na nchi kadhaa waitifaki wake ziliunda muungano eti wa kimataifa na kutuma majeshi huko Syria bila ya kibali cha Umoja wa Mataifa wala ruhusa ya serikali ya Damascus kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. 

Askari wa Uingereza huko Deir al-Zour

Katika taarifa yake ya leo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeashiria jinsi muungano huo wa Marekani unavyotumia mabomu yaliyopigwa marufuku ya fosforasi dhidi ya wanawake na watoto wa Syria na kusema kuwa, jinai zinazofanywa na muungano huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Taarifa hiyo pia imezitaka nchi zote duniani zisiiruhusu Marekani kutumia haki za binadamu kama wenzo wa kukandamiza irada na matakwa ya mataifa mengine ya dunia. 

 

Tags

Maoni