Dec 14, 2019 03:06 UTC
  • Kuwait: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haipasi kuwa chini ya vikwazo

Mwakilishi wa Kuwait katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haipasi kuwa chini ya vikwazo.

Mansour Ayyad Al-Otaibi ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Al Jazeera na kuongeza kuwa Kuwait haitaki kuona nchi jirani na ya Kiislamu kama vile Iran ikiwa chini ya vikwazo. Mwakilishi wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa amedai kuwa kuna dalili chanya na uwezekano wa kujiri mazungumzo ya pande mbili kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba pande hizo zinaweza kufikia maafikiano kwa ajili ya kurekebisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Madai hayo ya Mansour Al-Otaibi yametolewa katika hali ambayo viongozi wote wa Iran wamekataa kufanya mazungumzo ya aina yoyote na Marekani na tangu mwanzo Tehran imekuwa ikiitaka Washington kurejea kwanza kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kisha kuiondolea vikwazo vyake vya kidhalimu nchi hii.

Bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Matamshi ya mwakilishi huyo wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa kuhusiana na nafasi chanya ya kuaminika ya Iran kwa jirani, yametolewa katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitoa pendekezo la 'Amani ya Hormoz' kwa lengo la kuondoa tofauti na nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi. Kabla ya hapo pia Khaled Al Jarallah, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait alinukuliwa akisema kuwa nchi yake inachunguza mpango wa 'Amani ya Hormoz' uliowasilishwa na Rais Hassan Rouhani wa Iran. 

Tags