Jan 10, 2020 12:09 UTC
  • Ndege ya abiria ya Ukraine yawaka moto Tel Aviv, Israel

Ndege ya abiria aina ya Boing 737-800 ya Shirika la Ndege la Ukraine, imewaka moto katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv, Israel.

Tukio hilo la kuwaka moto injini ya upande wa kushoto wa ndege hiyo, limejiri sambamba na kujiri tukio la kuanguka ndege nyingine ya Boing 737-800 ya Shirika la Ndege la Ukraine mjini Tehran siku ya Jumatano. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika video iliyosambazwa na jeshi la zimamoto katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv, inawaonyesha maafisa wa jeshi hilo uwanjani hapo wakizima moto injini ya ndege hiyo. Hii ni katika hali ambayo asubuhi ya Jumatano iliyopita ndege ya Boing 737-800 mali ya Ukraine ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini (MA) mjini Tehran ambapo katika tukio hilo abiria 167 na wahudumu 9 walipoteza maisha.

Mabaki ya ndege ya Ukraine iliyoanguka mjini Tehran siku ya Jumatano

Hata hivyo Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada, baadhi ya viongozi wa Marekani na baadhi ya vyombo vya habari vya kigeni vilieneza propaganda chafu kuhusiana na ajali hiyo na kudai kuwa ndege hiyo ilianguka kufuatia kupigwa kombora na kwamba eti huenda shambulizi hilo halikufanyika kwa makusudi. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kutupilia mbali madai hayo bandia ya vyombo vya habari vya kigeni na viongozi wa Marekani, wameanzisha uchunguzi wa dharura kwa lengo la kubaini chanzo cha tukio hilo kwa kutegemea viwango vya kimataifa na sheria za Shirika la Kimataifa la Anga (ICAO).

Tags

Maoni