Jan 17, 2020 07:24 UTC
  • Askari wa US waliojeruhiwa na makombora ya Iran wanatibiwa Ujerumani na Kuwait

Licha ya utawala wa Washington hapo awali kudai kuwa hakuna askari wa Marekani aliyeuawa au kujeruhiwa katika majibu makali yaliyotolewa na Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq, lakini hivi sasa imefichuka kuwa, wanajeshi kadhaa wa US waliojeruhiwa walipekwa kwa usafiri wa ndege katika nchi za Ujerumani na Kuwait kwa ajili ya matibabu.

Kanali ya televisheni ya ABC News ya Marekani imewaonyesha askari 11 wa nchi hiyo wakitibiwa mjini Landstuhl nchini Ujerumani na katika kambi ya Arifjan nchini Kuwait.

Hapo jana, maafisa wa Marekani walilazimika kukiri juu ya kujeruhiwa wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali kukataa katakata kuwa kulikuwepo na majeruhi katika jibu hilo kali la Iran.

Masaa machache baada ya Iran kuvurumisha makombora na kupiga kambi mbili za kistrarajia za Marekani nchini Iraq, Rais Donald Trump alijitokeza na kudai kuwa, "ni furaha kuwatangazia Wamarekani kuwa hakuna askari wetu hata mmoja aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran nchini Iraq."

Wanajeshi wa Marekani wakimbeba mwenzao mwenye majeraha

Afisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH alisema kuwa, zaidi ya magaidi 80 wa jeshi la Marekani wameangamizwa na karibu 200 wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo ya makombora.

Siku chache baada ya majeshi ya kigaidi ya Marekani kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad tarehe 3 mwezi huu, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC lilishambulia kwa makumi ya makombora kambi za jeshi la Marekani katika mkoa wa Al-Anbar na Erbil nchini Iraq.

Tags

Maoni