Jan 17, 2020 12:16 UTC
  • Utawala wa katili wa Kizayuni wawashambulia Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza

Helikopta ya utawala wa Kizayuni wa Israel imevurumisha makombora ambayo yamelenga vituo vya makundi ya wapigania ukombozi (wanamuqawama) wa Palestina katika eneo la mashariki mwa Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa mashambulizi hayo yalitekelezwa usiku wa kuamkia Ijumaa ikiwa ni katika muendelezo wa mashambulizi ya hivi karibuni ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

Siku ya Jumatano pia  ndege za kivita za Israel zilishambulia makazi ya raia magharibi mwa Ghaza.  Utawala wa Kizayuni wa Israel unadai kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa maroketi ambayo yalivurumishwa na wanamapamabano wa Palestina kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Vyombo vya habari vya Palestina vinaripoti kuwa, kati ya maeneo yaliyolengwa ni kituo cha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Ndege za kivita za Israel zinalenga maeneo ya raia Ghaza

Tokea Disemba 2017, utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Kufuatia mashambulizi hayo ya Wazayuni maelfu ya Wapalestina wameuawa shahidi au kujeruhiwa. 

Tokea mwka 2006, utawala wa Kizayuni uliweka mzingiro katika Ukanda wa Ghaza kufuatia ushindi wa Hamas katika uchaguzi wa kidemokrasia. Mzingiro huo wa kinyama umesababisha eneo hilo kukumbwa na uhaba mkubwa wa dawa, chakula na mahitajio mengine muhimu.

 

Tags

Maoni