Jan 18, 2020 02:55 UTC
  • Mazungumzo eti ya amani kati ya Marekani na Taleban huko Qatar yavunjika

Waziri wa Serikali Katika Masuala ya Afghanistan, amesema kuwa mazungumzo eti ya 'amani' kati ya Marekani na kundi la Taleban yanayofanyika nchini Qatar, yamevunjika.

Salam Rahimi ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika Kabul, mji mkuu wa Afghanistan ambapo ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita duru 11 za mazungumzo hayo kati ya Taleban na Marekani mjini Doha, Qatar zimefanyika bila kuwa na natija ya kuridhisha. Akiashiria kwamba serikali ya Kabul imejiandaa kufanya mazungumzo na kundi la Taleban, Waziri wa Serikali Katika Masuala ya Afghanistan amebainisha kwamba wakati wowote ujumbe wa Marekani utakapopata taarifa ya mpango wa kupunguza vitendo vya utumiaji mabavu kutoka kwa kundi la Taleban, inaweza pia kufanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa wa Afghanistan.

Mwakilishi wa Marekani katika mazungumzo hayo yaliyofeli

Aidha Rahimi amesisitiza kwamba serikali ya Afghanistan inalitaka kundi la Taleban likubalia usitishaji vita ili kufanyike mazungumzo yatakayopelekea kupatikana amani ya kweli. Kabla ya hapo Taleban ilikuwa imetangaza kwamba iwapo mazungumzo hayo yatahusu suala la udhibiti wa Afghanistan, basi litakubali mazungumzo hayo ambayo yataifanya Marekani kutia saini makubaliano ya kuondoa askari wake kikamilifu katika ardhi ya nchi hiyo. Mazungumzo hayo yasiyo na maana na yaliyofeli kati ya Marekani na kundi la Taleban yamekuwa yakifanyika katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kutekelezwa mpango wa amani unaozingatia maslahi na thamani za kidini na za taifa la Afghanistan.

Tags

Maoni