Jan 19, 2020 04:34 UTC
  • Iraq: Hatua ya Marekani ya kujiondoa JCPOA, ndio chanzo cha mzozo Asia Magharibi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imesema kuwa hatua ya Marekani ya kujiondoa kwenye mapatano ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA ndio sababu kuu ya ongezeko la mzozo wa hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.

Mohamed Ali Alhakim, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha habari na Ayman Safadi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan mjini Baghdad ambapo pia sambamba na kuelezea udharura wa juhudi za Iraq katika vita na ugaidi amesema kuwa, mapambano na ugaidi sio suala la Iraq pakee, bali ni suala la kimataifa na kieneo. Ameongeza kwamba kushtadi mzozo katika eneo, kunaimarisha uwezo wa makundi ya kigaidi.

Trump, chanzo cha mizozo yote Asia Magharibi na duniani kwa ujumla

Kwa upande wake Ayman Safadi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan pia amesisitizia ulazima wa juhudi za pande zote kwa ajili ya kupunguza mizozo na kulinda usalama wa eneo na kubainisha kwamba, eneo la Asia Magharibi halihitaji vita vya wenyewe kwa wenyewe. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan amefanya ziara rasmi ya kikazi mjini Baghdad. Akiwa Iraq Ayman Safadi amekutana na Barham Salih, Rais wa Iraq, Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu na Mohamed al-Halbousi, Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Tags

Maoni