Feb 08, 2020 13:17 UTC
  • Barghuthi: Hatua za utawala wa Kizayuni hazitadhoofisha irada ya taifa la Palestina

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Palestina amesema, hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel haziwezi kudhoofisha irada ya taifa la Palestina.

Mustafa Barghuthi ametoa kauli hiyo kufuatia jinai za hivi karibuni zilizofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

Wapalestina wasiopungua watano wameuawa shahidi na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika makabiliano ya masaa 48 yaliyopita yaliyojiri kati ya askari wa Kizayuni na Wazayuni na Wapalestina wanaopinga mpango wa kidhalimu wa Marekani wa Muamala wa Karne.

Maandamano ya kulaani uitwao Muamala wa Karne

Barghuthi amebainisha kuwa, utawala unaoikalia Quds kwa mabavu umeshadidisha makusudi hatua kandamizi dhidi ya Wapalestina; na lengo la hatua zote hizo ni kutaka kuubadilisha mtazamo wa taifa la Palestina kuhusiana na njama ya Muamala wa Karne.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Palestina amesema, Wapalestina wamedhamiria kwa dhati kujikomboa kikamilifu na kupata uhuru wao kamili; na hatua za utawala wa Kizayuni zitaongeza tu maradufu muqawama wao wa kukabiliana na mpango wa Marekani uliopewa jina la Muamala wa Karne.../

 

Tags

Maoni