Feb 18, 2020 01:39 UTC
  • Jeshi la Syria: Tutang'oa mizizi ya ugaidi wa ukufurishaji

Jeshi la Syria sambamba na kuashiria kukombolewa makumi ya vijiji na miji ya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, limesisitiza kuendeleza mapambano yake kwa ajili ya kuung'oa ugaidi wa ukufurishaji.

Kamandi kuu ya jeshi la Syria imetoa taarifa hiyo na kubainisha kwamba, katika operesheni zake kadhaa zilizotekelezwa na jeshi hilo, limeweza kukomboa vitongoji na idadi kubwa ya makazi na viwanda vilivyokuwa vikidhibitiwa na magaidi. Aidha jeshi hilo limeongeza kuwa limefanikiwa kudhibiti vivuko vya viunga vya magharibi mwa mji wa Aleppo na miinuko yake ambayo ilikuwa mikononi mwa magaidi hao. Jeshi la Syria katika kuendeleza operesheni yake katika mji wa Aleppo sambamba na kukomboa maeneo ya Kafru Dael, Shikhun na Tal Sheikhun, limeangamiza idadi kubwa ya magaidi.

Raia wa Syria wakipongeza msaada wa Iran katika kuzima njama za magaidi na vibaraka wao

Jumamosi iliyopita pia jeshi hilo lilifanikiwa kukomboa vijiji viwili vya Ajel na Uwaijil pamoja na mji mdogo wa Arwam Al Kubra magharibi mwa mkoa wa Aleppo. Mgogoro wa Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, Saudia, Israel na Imarati kuivamia nchi hiyo ya Kiarabu kwa maslahi ya utawala haramu wa Kizayuni, njama ambazo hata hivyo zimeishia kufeli hadi sasa.

Tags

Maoni