Feb 19, 2020 11:38 UTC
  • Kesi ya Netanyahu yaiva; sasa kusikilizwa Machi 17

Kesi inayomkabili Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel na inayosubiriwa kwa hamu sasa inatarajiwa kuanza kusikilizwa tarehe 17 ya mwei ujao wa Machi.

Jana Jumanne Netanyahu alipokea barua inayomtaka afike mahakamani tarehe 17 ya mwezi ujao wa Machi kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, Netanyahu anatarajiwa kukiongoza chama chake cha Likud katika uchaguzi wa Bunge tarehe Pili mwezi ujao. Uchaguzi huo unafanyika kufuatia ule wa Aprili na Septemba mwaka jana kushindwa kuikwamua Israel katika kinamasi ilichokwama cha kuunda serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Israel Avichai Mandelblit

Benjamin Netanyahu anakabiliwa na mafaili manne ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Katika miaka ya hivi karibuni, mawakili wa Netanyahu na watu wenye uwezo na ushawishi mkubwa katika utawala wa Israel wamekuwa wakitumia ushawishi wao na hata vitisho ili kuhakikisha kuwa kesi hizo za ufisadi zinasitishwa au zinasitishwa kwa muda mahakamani.

Mwanasheria Mkuu wa Israel Avichai Mandelblit  alitangaza mwezi Novemba kuwa, Netanyahu amekuwa akimshinikiza sana ili asitangaze kuwa ana kesi za kujibu. Pamoja na kuwepo mashinikizo hayo, mwezi wa Novemba Mandelblit alimfungulia mashtaka Netanyahu kwa tuhuma za kupokea hongo, udanganyifu na kuvunja uaminifu. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya utawala bandia wa Israel kwa Waziri Mkuu aliye madakarani kufunguliwa mashtaka.

Maoni