Feb 21, 2020 07:12 UTC
  • Wanajeshi vamizi wa Marekani wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, SEPAH
    Wanajeshi vamizi wa Marekani wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, SEPAH

Maulamaa wa nchi mbalimbali za Kiislamu waliokutana nchini Yemen wamelaani jinai za Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kuhimiza kufurushwa kikamilifu mawanajeshi magaidi wa dola hilo la kibeberu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kikao cha kuipinga Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kilifanyika jana nchini Yemen kikiwashirikisha maulamaa kutoka Palestina, Lebanon, Syria, Yemen na Iraq.

Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya video kimemshirikisha pia Mufti Mkuu wa Syria, Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun aliyetoa hotuba ya kuunga mkono juhudi za kimataifa za kupambana na njama mpya za rais wa Marekani, Donald Trump za "Muamala wa Karne" ambazo zinalenga kuangamiza kikamilifu kadhia ya Palestina.

Kikao cha Maulamaa wa Kiislamu cha nchini Yemen kimewashirikisha maulamaa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu

 

Waliohutubia kikao hicho wamesema kuwa lengo la njama hizo mpya za Marekani ni kulinda uwezo wa dola pandikizi la Israel, kuzusha mizozo katika eneo hili, kupora utajiri wa nchi za Kiislamu na kuharakisha kampeni ya kuweko uhusiano wa kawaida baina ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mufti Mkuu wa Syria, Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun amezilaumu baadhi ya nchi za Kiarabu na kusema, inawezekana vipi nchi hizo za Kiarabu zinaruhusu anga zao kutumiwa na Wazayuni kupitishia ndege zao kuelekeza Israel lakini haziruhusu anga hizo kutumika kuwapelekea misaada ya dharura wananchi Waislamu na Waarabu wa Yemen?

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchni Syria

Taarifa ya mwisho wa kikao hicho imelaani jinai za Marekani za kuwaua kiholela na kidhulma Waislamu huku jinai ya karibuni kabisa ikiwa ni ile ya kuwaua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq, maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi.

Tags

Maoni