Feb 25, 2020 01:22 UTC
  • Kesi za kwanza za Corona zaripotiwa Iraq, Kuwait, Bahrain na Afghanistan

Iraq, Kuwait, Bahrain na Afghanistan zimeripoti kesi za kwanza za ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona katika nchi hizo za eneo la Asia Magharibi.

Kuwait imeripoti kesi tatu za maradhi hayo ambayo yanajulikana pia kana Covid-19. Kesi moja moja za Corona zimeripotiwa katika nchi za Iraq, Bahrain na Afghanistan.

Baada ya kuripotiwa kesi hizi mpya katika nchi hizo nne, idadi ya nchi za Asia Magharibi zilizothibitisha kuwa na ugonjwa wa Corona kufikia sasa ni nane.

Huku hayo yakiarifiwa, idadi ya walioaga dunia kutokana na virusi hivyo hatarishi nchini Italia imeongezeka na kufikia watu watano, huku idadi ya waathirika ikiongezeka pia na kupindukia watu 200.

Hatua za tahadhari Iran. Corona imeua watu 12 nchini

Kadhalika China ambayo ni kitovu cha virusi hivyo imeripoti vifo vipya 150, huku serikali ya Beijing ikitangaza kuakhirisha vikao vya Bunge kutokana na ugonjwa huo. Aidha Korea Kusini imeripoti kesi mpya 70, na kufikisha idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa zaidi ya 800 nchini humo.

Hadi sasa watu wasiopungua 79,000 wameambukizwa Corona kote duniani, aghalabu wakiwa nchini China huku wengine wasiopungua 2,600 wakipoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

 

Tags