Feb 27, 2020 13:00 UTC
  • Saudia yasimamisha Umrah kwa hofu ya virusi vya Corona

Saudi Arabia imetangaza kusimamisha kwa muda Ibada ya Umrah katika Msikiti wa Mtume Muhammad SAW mjini Madina kutokana na hofu ya kuenea virusi vya Corona ambavyo vimeua maelfu ya watu kufikia sasa.

Katika ujumbe wa Twitter mapema Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema Ibada hiyo ya kuuzuru Msikiti wa Mtume Mtukufu mjini Madina imesimamishwa kwa muda ili kuzuia kuenea virusi hivyo.

Taarifa hiyo imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kulinda maisha ya raia wa Saudi Arabia na pia wale wanaosafiri nchini humo kwa ajili ya Umrah au utalii.

Waumini wakitufu katika Kaaba mjini Makkatul Mukarramah, Saudia

Homa ya virusi vya Corona iliripotiwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan mkoani Hubei mashariki mwa China Disemba mwaka uliopita 2019 mbali na kuathiri mikoa 35 ya nchi hiyo homa hiyo imeenea katika zaidi ya nchi 50 zikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Australia, Italia, Thailand, Korea Kusini, Japan, Canada, Ufaransa na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Watu zaidi ya 2,800 wamefariki dunia hadi sasa hususan nchini China kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo hatarishi.

Maoni