Feb 27, 2020 13:11 UTC
  • Risasi za jeshi la Israel zawapofusha Wapalestina 21 Ukanda wa Gaza

Kituo cha Haki za Binadamu cha Beytulahm (Bethlehem) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kimeripoti kuwa, Wapelestina 21 katika Ukanda wa Gaza wamesababishiwa upofu na ufyatuaji risasi wa jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya miaka miwili iliyopita.

Shirika la habari la Fars limeripoti hayo na kuongeza kuwa, katika mwaka 2018 na 2019, Wapalestina 19 walipoteza jicho moja kila mmoja baada ya kushambuliwa na wanajeshi wa Israel katika maandamano ya Haki ya Kurejea karibu na uzio unaotenganisha Gaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Habari zaidi zinasema kuwa, Wapalestina wengine wawili walipoteza macho yao mawili katika hujuma hizo za askari wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika kila Ijumaa katika mpaka wa Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tokeش mwaka 1976.

Jeshi la Israel linaendeleza ukatili mkabala wa kimya cha jamii ya kimataifa

Wapalestina zaidi ya 330 wameuawa na wanajeshi wa utawala wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza, huku wengine 31,000 wakijeruhiwa tangu yalipoanza maandamano hayo ya 'Haki ya Kurejea' mnamo Machi mwaka 2018.

Hadi leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuziyahudisha ardhi hizo na kufuta kabisa utambulisho wake wa Kiislamu-Kipalestina.

Tags

Maoni