Mar 25, 2020 12:16 UTC
  • Idadi ya waathirika wa Corona yaongezeka ndani ya Israel

Idadi ya waathirika wa virusi vya Corona kati ya Wazayuni, imefikia 1930 baada ya kusajiliwa kesi mpya 488.

Katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, Wazayuni wengine wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo, ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel). Jumanne iliyopita jeshi la utawala haramu wa Kizayuni lilithibitisha kwamba askari wengine watano wameambukizwa virusi vya Corona na kwamba jumla ya askari walioambukizwa ugonjwa huo ndani ya jeshi hilo imefikia 25.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zaidi ya askari elfu sita wa utawala wa Kizayuni wamewekwa karantini hadi sasa. Aidha Jumanne usiku Benjamin Tetanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Israel alionya kwamba inakadiriwa kuwa mwezi mmoja ujao karibu watu milioni moja kati ya watu wote milioni nane na 600 wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wataambukizwa virusi vya Corona na karibu watu elfu 10 watapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Tags

Maoni