Mar 26, 2020 04:35 UTC
  • Harakati ya Hizbullah ya Iraq yafichua njama mpya za Marekani nchini humo

Harakati ya Hizbullah ya Iraq ambayo ni sehemu ya makundi kadhaa ya kujitolea ya wananchi yanayounda Harakati ya 'Hashdu sh-Sha'abi' imetahadharisha kuhusiana na juhudi za Marekani za kutekeleza njama hatari dhidi ya Iraq na kuwataka wanamuqawama wa nchi hiyo kukabiliana na nia na malengo machafu ya adui Mmarekani.

Taarifa hiyo ya Hizbullah imefichua njama mpya ya Marekani ya kutaka kushambulia maeneo ya jeshi na ya makundi ya muqawama nchini humo wakati huu wa kuenea kwa virusi vya Corona. Kwa mujibu wa taarifa hiyo njama hiyo inajumuisha utekelezaji wa operesheni za kijeshi dhidi ya kambi za jeshi la Iraq na Hashdu sh-Sha'abi kwa kutumia jeshi la anga na nchi kavu. Sambamba na kubainisha kuwa nafasi ya Marekani nchini Iraq inatishia usalama na uthabiti wa nchi hiyo, Harakati ya Hizbullah imesisitiza kuwa makundi ya muqawama hayatazingatia mistari yoyote miekundu iwapo watenda jinai wa Kimarekani watatekeleza hatua yao hiyo na kwamba taasisi zote za kijeshi, kiusalama na kiuchumi za nchi hiyo ndani ya Iraq hazitasalimika na radiamali ya wanamuqawama. Inafaa kuashiria kuwa, hadi sasa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zimetekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya maeneo ya jeshi la Iraq na Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Askari vamizi wa Marekani nchini Iraq

Aidha baada ya mafanikio makubwa ya harakati hiyo ya wananchi katika vita vyake dhidi ya genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), Marekani na Israel zimekuwa zikitekeleza njama mbalimbali zenye lengo la kuiwekea mashinikizo zaidi harakati hiyo. Harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ambayo ni moja ya mirengo muhimu ya muqawama, imekuwa na nafasi kubwa katika kukabiliana na njama na hatua chafu za Marekani na utawala bandia wa Kizayuni katika eneo.

Maoni