Apr 07, 2020 08:17 UTC
  • UN yapinga madai ya kuhusika Syria katika shambulizi dhidi ya hospitali za Idlib

Kamati ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imepinga madai kwamba Syria imeshambulia hospitali na vituo vya afya huko Idlib.

Ripoti iliyotolewa leo na kamati hiyo ya UN inayochunguza masuala makhsusi ikiwa ni pamoja na madai kuwa Syria imeshambulia taasisi za kiraia, imesema kuwa, haijapata ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba serikali ya Syria imehusika na mashambulizi dhidi ya hospitali zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa huko Idlib.

Ripoti hiyo imeashiria shambulizi lililolenga hospitali ya Kafr Nabl na kusisitiza kuwa, hadi sasa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani mtu au kundi lolote kuhusiana na shambulizi hilo. 

Wakati huo huo kamati hiyo imethibitisha kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba makundi ya kigaidi ndiyo yaliyoshambulia kambi ya wakimbizi huko kaskazini mwa Syria. 

Ripoti ya kamati hiyo imekabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. Umoja wa Mataifa uliunda kamati hiyo mwezi Juni mwaka 2019 kwa shabaha ya kufanya uchunguzi kuhusiana na mashambulizi yaliyolenga taasisi za kiraia katika mkoa wa Idlib nchini Syria. 

Tags

Maoni