Apr 08, 2020 03:39 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah: Utawala wa Kizayuni una wasiwasi kuwa uhai wake hautazidi miaka 80

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, hivi sasa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu kuna utawala ghasibu ambao una wasiwasi wa kulinda uwepo wake wa kisiasa na una hofu kuwa uhai wake hautazidi miaka 80.

Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, akiashiria hofu na wasiwasi walionao Wazayuni juu ya kudhihiri Imam Mahdi (Ajjala-Allahu Ta'ala Farajahu-Sharif), katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kukaribia Shaaban 15, siku ya kuadhimisha mazazi yenye baraka ya mtukufu huyo ambaye ni Imam wa 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Sayyid Hassan Nasrullah ametoa mkono wa heri na pongezi kwa mnasaba wa siku hiyo yenye baraka na kueleza kwamba, kuzaliwa kwa Imam Mahdi (as) ni sawa na kuanza kukaribia zama za kuthibiti ahadi ya Mwenyezi Mungu; na akaongezea kwa kusema: Atakapodhihiri Imam Mahdi (Allah Aharakishe Kudhihiri Kwake) ataujaza ulimwengu uadilifu, amani na upendo.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ametoa mkono wa pole pia kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku aliyouawa shahidi Ayatullah Muhammad Baqir Sadr pamoja na ndugu yake wa kike Bintul-Huda kwa amri  ya dikteta wa Iraq Saddam; na akamuenzi na kumtaja Ayatullah Sadr kuwa ni mwanafalsafa na mwanafikra mkubwa.

Shahidi Ayatullah Muhammad Baqir Sadr (kushoto) na Shahidi Amina Haydar al-Sadr (Bintul-Huda Sadr)

Sayyid Hassan Nasrullah alinukuu maneno aliyosema shahidi Sadr kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (MA) na akasema: Wakati Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipopata ushindi, shahidi Sadr alisema: Imam Khomeini (as) amewezesha kuthibiti lile walilokuwa wakilitaka Manabii.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amenukuu maneno mengine pia aliyotamka shahidi Ayatullah Muhammad Baqir Sadr alipousia kwa kusema: "Yeyukieni kwa Imam Khomeini kama yeye Imam alivyoyeyukia kwenye Uislamu" na akasisitiza kuwa, ufuataji wa wasia huo na njia hiyo utaendelea.../

Maoni