Apr 08, 2020 08:03 UTC
  • Arab League yatahadharisha kuhusu hatua ya Israel ya kulitumia vibaya janga la Corona

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amezungumza kwa simu na Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na kutahadharisha kuhusu hatua ya Israel ya kutumia vibaya janga la virusi vya corona.

Ahmad Abu Ghait jana alifanya mazungumzo ya simu na Saib Uraiqat kuhusu kutumia vibaya Israel janga la virusi vya corona kwa ajili ya kuziunganisha na ardhi yake ardhi mpya za Palestina na pia kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. 

Katika mazungumzo hayo ya simu kati ya Katibu wa Kamati ya Utendaji ya PLO na Katibu Mkuu wa Arab League wawili hao wamebadilishana mawazo kuhusu hatua za kitiba zilizochukuliwa katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan na Ukanda wa Ghaza kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya corona. 

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na Ben Gantz kiongozi wa Muungano wa Bluu- Nyeupe hivi karibuni waliafikiana kuhusu kuanzishwa mamlaka ya utawala huo katika bonde la mto Jordan na katika vitongoji vilivyopo katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan katika fremu ya mapatano kwa ajili ya kuunda serikali ya mseto.  

Ben Gantz na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu 

Katika kampeni za uchaguzi mwaka jana Netanyahu aliahidi kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibii na bonde la mto Jordan na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ili kwa kiasi fulani ili aweze kufungua njia ya uchaguzi na kuasisi serikali ambayo imekwama kwa karibu mwaka mmoja sasa. 

 

 

Tags

Maoni