Apr 09, 2020 02:43 UTC
  • Wakazi wa Al-Hasakah nchini Syria wawalazimisha askari wa Marekani kurudi nyuma

Wakazi wa kijiji cha 'Kharab Askar' katika mkoa wa Al-Hasakah, kaskazini mashariki mwa Syria kwa mara nyingine tena wamewazuia askari wa Marekani na kuwalazimisha kurudi nyuma.

Siku ya Jumanne wakazi wa kijiji cha Kharab Askar cha mji wa Qamishli wakishirikiana na askari wa jeshi la Syria walizuia kuingia magari ya deraya ya askari vamizi wa Marekani na wapiganaji kadhaa wa Kikurdi, ndani ya kijiji hicho, sambamba na kuwalazimisha kurudi nyuma. Katika upande mwingine, msafara wa magari ya deraya wa askari wa Marekani uliokuwa unakaribia kufika kwenye kituo cha upekuzi cha kijiji cha 'Hamu' katika mji wa Qamishli, ulizuiliwa na wakazi wa kijiji hicho waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo hicho na hivyo kuufanya ushindwe kuingia eneo hilo.

Wananchi wa Syria wanakaribisha msaada wa Iran na Russia dhidi ya magaidi

Raia hao wa Syria wanapinga uwepo wa askari vamizi wa Marekani na ulio kinyume cha sheria katika ardhi yao. Hadi sasa wakazi wa vijiji vya mji wa Qamishli katika mkoa wa Al-Hasakah wamezuia mara kadhaa misafara ya askari vamizi wa Marekani kuingia vijiji hivyo. Aidha mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu wakazi wa vijiji hivyo waliushambulia kwa mawe msafara wa askari hao wa Marekani na kuwalazimisha kurudi nyuma.

Tags

Maoni