May 23, 2020 02:35 UTC
  • Kamati za muqawama za Palestina zapongeza hotuba ya Kiongozi Muadhamu Siku ya Quds

Msemaji wa Kamati za Muqawama za Palestina amesema kuwa, hotuba iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ni endelevu, ya kiwango cha juu na muhimu sana.

Abu Mujahid, Msemaji wa Kamati za Muqawama wa Palestina amesema hayo alipohojiwa na televisheni ya al Mayadeen na kuongeza kuwa, hotobu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa jana Ijumaa ni ya kiwango cha hali ya juu, endelevu na iliyobaba ujumbe wa kila namna kwa adui Mzayuni na Marekani.

Aidha amesema, makundi ya Palestina yanauangalia kwa jicho zuri uamuzi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina wa kusimamisha ushirikiano wake wa kiusalama na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesema, hatima ya kambi inayotafuta mapatano na Israel ni maangamizi na kusisitiza kuwa, kambi ya muqawama inazidi kuwa imara na kupata ushindi na heshima, siku baada ya siku.

Abu Mujahid

 

Jana Ijumaa, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa hotuba muhimu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na ndani ya hotuba hiyo mlikuwa na nasaha saba muhimu kuhusu jihadi kubwa na takatifu inayoendelea hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Miongoni wa nasaha hizo ni kuhakikisha kadhia ya Palestina haifanywi kuwa ya Wapalestina peke yao au ya Waarabu tu, bali ni kadhia ya kila Muislamu na kila mpenda haki duniani; wajibu wa kukombolewa ardhi zote za Palestina bila ya kubagua; kuepuka kuyaamini na kuyategemea madola ya kibeberu na dhalimu ya Magharibi na nasaha nyingine kadhaa muhimu sana.

Maoni