May 23, 2020 08:06 UTC
  • PFLP: Hotuba ya Kiongozi Muadhamu imeainisha ramani ya njia ya kuikomboa Palestina

Afisa wa ngazi za juu wa Palestina amesema hotuba ya jana ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds imechora na kuanisha ramani ya njia ya ukombozi wa Palestina.

Ahmad Abu Fuad, Naibu Katibu Mkuu wa Harati ya Ukombozi wa Palestina Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) amesema hayo katika mazungumzo yake na kanali ya televisheni ya Al Mayadeen ya Lebanon na kuongeza kuwa, "misimamo yote iliyoakisiwa na Ayatullah Ali Khamenei kwenye hotuba yake inaendana na matakwa ya Wapalestina."

Amempongeza Kiongozi Muadhamu kwa kuanisha ramani ya njia ya kuikomboa Palestina kupitia muqawama na mapmbano na kueleza bayana kuwa, "hili ndilo chaguo letu."

Katika hotuba yake ya jana Ijumaa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo huadhimishwa katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kila mwaka kote duniani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema mapambano ya kukombolewa Palestina ni wajibu na lengo la kila Muislamu na kwamba kila mmoja anapaswa kusaidia katika jitihada hizo takatifu za taifa la Palestina.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ndani ya hotuba hiyo ya Ayatullah Ali  Khamenei, mlikuwa na nasaha saba muhimu kuhusu jihadi kubwa na takatifu inayoendelea hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu ya kulikomboa taifa la Palestina.

Kadhalika aliashiria juu ya kubuniwa kwa donda la saratani la Uzayuni na kusisitiza kwamba mhalifu mkuu wa maafa ya Palestina ni serikali za nchi za Magharibi na siasa zao za kishetani.

 

Tags

Maoni