May 23, 2020 09:16 UTC
  • Uturuki yawatumia magaidi wa Syria msafara mwingine wa kilojistiki

Duru za habari za Syria zimeripoti kuwa, Uturuki imewatumia magaidi wa Syria msafara mwingine wa vifaa vya kijeshi katika maeneo unayoyakalia kwa mabavu ya kaskazini mwa Syria.

Shirika la habari la SANA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, jana mchana, Uturuki ilituma malori na magari 30 ya deraya yenye zana zote za kijeshi katika radhi za kaskazini mwa Syria zinazokaliwa kwa mabavu na Uturuki katika mkoa wa al Hasakah.

Tarehe 18 Mei pia, Uturuki iliimarisha uvamizi wake wa kijeshi katika nchi jirani ya Syria kwa kuweko ukanda inaodai ni wa amani katika eneo la Ra's al Ain, kaskazini mwa Syria.

Wanaejshi vamizi wa Uturuki nchini Syria

 

Uturuki imeyafamia maeneo ya kaskaizni mwa Syria na kuyakalia kwa mabavu maeneo hayo kwa madai ya kupambana na magaidi. Hadi hivi sasa wanajeshi wa Uturuki wako kwenye maeneo hayo.

Kitendo cha Uturuki cha kuyavamia maeneo ya kaskazini mwa Syria na kuyaunga mkono baadhi ya magenge ya kigaidi kunaendelea kulaaniwa vikali na duru mbalimbali kote ulimwenguni.

Tags

Maoni