May 24, 2020 07:57 UTC
  • Askari wa Kizayuni washambulia Wapalestina katika Swala ya Idi

Wanjeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina waliokuwa wamefika katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds kwa ajili ya ibada.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, wanajeshi wa utawala ghasibu siku ya Jumapili  asubuhi waliwashambulia  Wapalestina waliokuwa wamefika kando kando ya msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Swala ya Idi.

Pamoja na kuwepo utumiaji mabavu wa askari wa Kizayuni, Wapalestina hao hatimaye waliweza kuswali Swala ya Idul Fitr katika Medani ya Al Ghazala katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika lango la Babul Asbaat la msikiti huo.

Msikiti wa Al Aqsa

Eneo la ndani la Msikiti wa Al Aqsa limefungwa kwa muda wa miezi miwili sasa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 na kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Palestina, msikiti huo utafunguliwa kikamilifu baada ya siku kuu ya Idul Fitr.

Leo Jumapili, tarehe Mosi Shawwal ni siku kuu ya Idul Fitr katika aghalabu ya nchi za dunia. 

 

Tags

Maoni