Jul 10, 2020 02:24 UTC
  • Uturuki yavamia tena ardhi ya Syria, mara hii msafara wa malori 70 ya kijeshi waingia mkoani Idlib

Misafara mitatu ya jeshi la Uturuki ya malori yaliyosheheni zana za kijeshi imevuka mpaka wa mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria na kuingia ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

Asasi inayojulikana kama shirika la kutetea haki za binadamu la Syria imeripoti kuwa misafara hiyo ya jeshi la Uturuki ya malori 70 yaliyobeba zana za kijeshi imevuka kivuko cha mpakani cha Kafr Lusin na kuingia mkoani Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.

Mnamo mwezi Mei 2020 pia, Uturuki iliingiza mara mbili makumi ya malori na magari yaliyobeba zana za kijeshi na kilojisitiki katika ardhi ya Syria kupitia kivuko cha al -Adwaniyyah, magharibi mwa mji wa Raasul-Ain mkoani Hasakah.

Eneo la mpaka wa pamoja wa Uturuki na Syria

Kwa kutumia kisingizio cha kupambana na magaidi, Uturuki imevamia na kukalia kwa mabavu sehemu ya maeneo kadhaa ya kaskazini mwa Syria na hadi sasa kundi moja la askari wa jeshi la nchi hiyo lingali limepiga kambi katika maeneo hayo.

Uchokozi na uvamizi uliofanywa na Ankara katika eneo la kaskazini ya ardhi ya Syria na uungaji mkono wake kwa baadhi ya makundi ya kigaidi yaliyoko nchini humo umelaaniwa vikali na kukosolewa sana kimataifa.../

Tags

Maoni