Aug 03, 2020 03:39 UTC
  • Waziri wa Ulinzi: Lebanon iko tayari kukabiliana na hujuma ya utawala wa Kizayuni

Waziri wa Ulinzi wa Lebanon amesema jeshi la nchi yake liko tayari kabisa kukabiliana na uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Bi. Zeina Akar, Waziri wa Ulinzi wa Lebanon amenukuliwa akisema serikali ya Lebanon haijapuuza matukio ya hivi karibuni katika mpaka wa nchi hiyo na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kuongeza kuwa, Lebanon inalaani uvamizi wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni na inautazama uchokozi huo kuwa ni wenye kutishia uthabiti wa kusini mwa Lebanon. Akar ameongeza kuwa adui Muisraeli hukiuka mipaka ya Lebanon kila siku mbali na kikiuka maelfu ya mara azimo nambari 1701 la Baraza la Usalama. Amesema taarifa zote za wizara za serikali zilizopita na ya sasa ya Lebanon zinasisitiza kuhusu muqawama na kusimama kidete mbele ya maadui.

Waziri wa Ulinzi wa Lebanon aidha ameelezea matumaini kuhusu kuongoezwa muhula wa kuhudumu Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (UNIFIL) katika mpaka wa Lebanon na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel). Amesema muhula wa UNIFIL unapaswa kuongezwa bila kubadilisha majukumu ya kikosi hicho.

Askari wa UNIFI

Marekani inajaribu kubadilisha majukumu ya UNIFIL nchini Lebanon ili kikosi hicho kitumike dhidi ya Hizbullah.

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel Jumatatu iliyopita lilikiuka mamlaka ya kujitawala ya Lebanon na azimio 17 la Baraza la Uslama kwa kuvamia miinuko ya Kafr Shuba ya Lebanon na Mashamba ya Shebaa yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Tags

Maoni