Aug 04, 2020 17:09 UTC

Mlipuko mkubwa umeutikisha mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Mlipuko huo umejiri leo jioni karibu na Bandari ya Beirut na inahofiwa kuwa watu wasiopungua 10 wamefariki.

Shirika Rasmi la Habari la Lebanon limetangaza kuwa mlipuko huo umejiri katika ghala nambari 12 la Bandari ya Beirut na kwamba sababu ya moto ni mada za milipuko ambazo zilkuwa zimehifadhiwa hapo.

Mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kusikika kilomita nyingi kutoka eneo la tukio.

Taarifa za awali zinasema zaidi ya watu 150 wamejeruhiwa na kwamba wanapata matibabu hospitalini.

Kwa mujibu wa taarifa, mlipuko huo umesababisha hasara kubwa kwa nyumba za makazi na pia katika idara binafsi na za serikali. 

Tags

Maoni