Aug 05, 2020 02:34 UTC
  • Ukosoaji wa Waziri Mkuu wa Pakistan wa kuendelea mashambulio ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen

Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan amekosoa hatua ya Saudi Arabia ya kuendeleza hujuma na mashambulio yake ya kijeshi dhidi ya Yemen.

Akihojiwa na Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera, Imran Khan ametoa radiamali yake kwa kuendeea hujuma ya kijeshi ya Saudia dhidi ya Yemen na kusema kuwa, nchi hiyo inakabiliwa na maafa ya kibinadamu. Waziri Mkuu wa Pakistan ameashiria pia uharibifu mkubwa uliofanywa huko Yemen kufuatia hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia na kueleza kuwa, Islamabad inafanya juhudi kuhakikisha mashambulio na vita nchini Yemen vinafikia tamati.

Mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande upande nchi hiyo. Moto wa vita uliowashwa na Saudia na waitifaki wake nchini Yemen hadi sasa umeshasababisha makumi ya maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Ukosoaji wa Waziri Mkuu wa Pakistan dhidi ya kuendelea hujuma ya mauaji ya Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen ambayo imeingia mwaka wake wa sita ni ishara ya stratijia ya kueleweka ya Islamabad kuhusiana na vita vya Yemen.

Katika miezi ya awali ya kuanza uvamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen, viongozi wa Riyadh waliitaka serikali ya Pakistan iungane na Saudia katika vita hivyo, ombi ambalo lilikabiliwa na upinzani wa Bunge la nchi hiyo. Katika kukabiliana na pigo hilo la kuishawishi Pakistan iungane nayo katika vita vya Yemen, Riyadh ilifanya juhudi za kuiridhisha Islamabad kupitia ahadi kemkemu kama kuipatia mkopo na misaada isiyo na masharti. Hata hivyo kupitia hayo pia Saudia ilishindwa kufikia malengo yake.

Pamoja na hayo, baada ya Saudia kugonga mwamba kutokana na upinzani wa wazi wa Bunge la Pakistan kwa pendekezo lake la kutaka jeshi la nchi hiyo lishiriki katika vita vya Yemen, iliamua kupitia mlango wa uani ambapo ilianzisha juhudi za kutaka kufikia makubaliano ya siri na Imran Khan ili Pakistan iunge mkono vita vya Riyadh huko Yemen.

Hata hivyo kwa kuzingatia baadhi ya masuala ya kitaifa na ya kichama, Imran Khan hakukubaliana na ombi hilo la Saudia. Hasa kwa kuzingatia kuwa, baada ya kutangazwa wazi takwa la Saudia kwa Pakistan la kuitaka nchi hiyo ishirikiane na utawala wa Aal Saud katika vita dhidi ya Yemen kuliibuka upinzani wa wananchi na vyama pinzani kwa serikali ya Imran Khan vikakionya chma tawala cha Tahreek-e-Insaf kuhusiana na suala hilo.

Jinai za Saudi Arabia nchini Yemen

Sahibzadeh Hamid Saeed Kazmi, Waziri wa zamani wa Masuala ya Dini wa Pakistan na mmoja wa viongozi wa Chama cha Wananchi anasema:

Muungano wa kijeshi wa Saudia katika vita vya Yemen, upo kwa ajili ya kuhudumia Marekani tu na umeundwa kwa ajili ya maslahi ya dola hilo la Kimagharibi; na Pakistan kujiunga na muungano huo hakutakuwa na jingine ghairi ya kutoa huduma kwa Marekani na watawala wa Aal Saud.

Hata hivyo chini ya mashinikizo makali ya Saudia, Jeneral Raheel Sharif kamanda wa zamani wa Jeshi la Nchi Kavu la Pakistan aliongoza muungano wa kijeshi ulioshindwa wa vita dhidi ya Yemen, ambapo suala hilo lilikabiliwa na radiamali kali ya wananchi na duru za kisiasa na kihabari za Pakistan.

Kwa kuzingatia azimio la Bunge la Pakistan la Aprili 2016 ambapo nchi hiyo inapaswa kutokuwa upande wowote katika vita vya Yemen, uwepo wa jenerali Raheel katika muungano huo ulikuwa ukikiuka azimio hilo.

Hujuma ya kijeshi ya saudi Arabia inavyofanya uharibifu nchini Yemen

Licha ya kuwepo baadhi ya upendeleo kama kupatiwa misaada ya kifedha na Saudia, serikali ya Pakistan licha ya kukabiliwa na nakisi ya bajeti, lakini Imran Khan amekataa katakata kuungana na watawala wa Riyadh katika vita vyao huko Yemen.  

Imran Khan anaamini kuwa, kuwa pamoja na hatua yoyote ile ya Saudia katika vita dhidi ya Yemen kutachochea ukosefu wa uthabiti wa kisiasa na ndio maana hajaruhusu chama chake tawala cha Threek-e-Insaf kichukue hatua ambayo inakidhi matarajio ya Riyadh. Katika mazingira kama haya, Imran Khan tangu achukue usukani wa Waziri Mkuu mwaka 2018, hii ni mara ya kwanza kutangaza wazi na kukosoa vita vya Saudia dhidi ya Yemen.

Tags

Maoni